Friday, November 4, 2011

Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma Balozi Juma Mwapachu(katikati) akitembelea Chuo hicho leo  katika ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe na Rais kushika nafasi hiyo .wengine kulia ni Prof Ludovick Kinabo na kushoto ni Dr Rex  J .Kidyalla mkurungenzi wa Maktaba UDOM



 Mwenyekiti Mpya  Baraza  la Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) Balozi Juma Mwapachu akiongea na Wanafunzi wa  Chuo  cha Sayansi  ya  Tiba  alipotembelea Chuo hapo leo

Mwenyekiti  Mpya wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) akitembelea  baadhi ya meneo ya Chuo hicho kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa na Mhe Rais hivi karibuni
(Picha zote na Ibrahim  Joseph)
.

Wednesday, November 2, 2011

PICHA ZA MECHI KATI POLISI NA YANGA

Mshambuliaji wa Yanga Mghana Keneth Asamoah akishangilia baada ya kufunga bao lake kwenye mechi yao na Polisi Tanzania ilichezwa  katika uwanja wa Jamhuri Dodoma ,Yanga walishinda goli 1-0

Beki wa timu ya Polisi Tanzania Eliasa Mashaka (kushoto) akijaribu kumzuia Mchezaji wa Yanga Mzambia Devis Mwape kwenye mechi yao ilichezwa uwanja wa Jamhuri Dodoma

Wachezaji wa Timu ya Yanga wakimpongeza mchezaji mwenzao Keneth Asamoah (katikati)baada ya kuifungia timu yao goli pekee walipocheza na timu ya Polisi Tanzania katika uwanja wa Jamhuri Dodoma

MAANDALIZI YA KILOMO

Bibi Roda Andrea (75) Mkazi wa Hombolo Bwawani kambi  wenye ukoma ya Samaria akiandaa shamba kwa ajili ya kilimo kama alivyokutwa na mpiga picha Kijijini hapo leo

Tuesday, November 1, 2011

Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Dr
Rehema Nchimbi (kulia) akiongea na Waandishi wa Habari  wa Mkoa wa  Dodoma   kwenye Mkutano ulifanyika Ofisini  kwake jana