PICHA NA IBRAHIM JOSEPH
Tarehe 20/oct/2011
Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 11 waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa wameachiwa kwa Dhamana jana usiku baada ya kuwekewa Dhamana na Wanachama wa Chama hicho .
Viongozi hao walikamatwa jana mchana katika viwanja vya barafu Mkoani hapa na Polisi baada ya kutaka kuanza maandalizi ya mkutano wa hadhara walioumbea kibali tangu tarehe 16 mwezi wa kumi mwaka huu.
Waliokamatwa ni Mkurugenzi wa Taifa wa Operesheni na mafunzo wa CHADEMA Benson Kigaila na baadhi ya Viongozi wa ngazi ya Mkoa na Wilaya na Baadhi ya Wanachama wa Chama hicho.
Akiongea na Wandishi wa Habari Mkoani hapa baada ya kuachiwa kwa Dhamana, Mkurugenzi wa Taifa wa Operesheni na mafunzo wa CHADEMA Benson Kigaila alisema wao waliwandikia Polisi barua ya kuwataarifu kuwa wana mkutano wa hadhara tarehe 19 mwezi huu kama sheria ya uchaguzi inavyoelekeza kuwa utoe taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).
Alisema cha kushangaza polisi waliwaletea barua ya kuzuia mkutano wao tarehe hiyo ya Mkutano majira ya saa 5 na wakati Jeshi hilo wanajua wameshaingia gharama za matangazo ya mkutano wao wa hadhara na kukodisha viti pamoja na gari la matangazo .
Kigaila alisema katika barua hiyo ya Polisi ilieleza kuwa sababu za kuuzuia mkutano wa Chadema ni kuwa Jeshi hilo waligundua kuwa kama mkuutano huo ungefanyika kungekuwa na uvunjifu wa Amani .
Alisema kama Polisi waligundua kuna uvunjifu wa Amani kwa nini Polisi wasilete Askari wengi kulinda Mkutano na matokeo yake walileta gari nne za Jeshi la Polisi kuzuia wanachama wa Chama hicho wasifanye Mkutano si wangetumika kusimamia huo mkutano wakiona kuna jambo linataka kutokea basi wangeuzuia na kuwahukumu kwa hisia zao
Akielezea zaidi Kigaila alisema sababu za kukamatwa kwao na Polisi ni makosa makuu mawili ,moja ni kukiuka Amri halali ya Polisi na lingine ni kutaka kufanya mkutano bila kibali halali cha Polisi.
Kigaila alisema chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakiana muda wa kulumbana na Watu wanaotumiwa na vyama vingine kukivuruga chama chao bali wao wanaendel;ea na harakati zao za kutetea maslahi ya Wanyonge .
Mkurungenzi huyo wa CHADEMA alisema wameachiwa kwa Dhamana na hawajui kama Polisi watawafungulia kesi au vipi ila wao kama Chama wanahitaji mkutano wa hadhara kama barua yao ilivyoomba na hawahitaji kulubana na Jeshi hilo kwani jeshi hilo lipo kwa kuwalinda Watanzania na sio kusababisha vurugu.
mwisho