Thursday, October 20, 2011

VIONGOZI WA CHADEMA WACHIWA NA POLISI DODOMA

PICHA NA IBRAHIM  JOSEPH
Tarehe 20/oct/2011

Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 11 waliokuwa wanashikiliwa  na Jeshi la Polisi Mkoani hapa wameachiwa kwa Dhamana jana usiku baada ya kuwekewa Dhamana na Wanachama wa Chama hicho .

Viongozi hao walikamatwa jana mchana  katika viwanja vya barafu Mkoani hapa  na Polisi  baada ya kutaka kuanza maandalizi ya mkutano   wa  hadhara walioumbea kibali tangu tarehe 16 mwezi wa kumi  mwaka huu.


Waliokamatwa ni Mkurugenzi wa Taifa wa  Operesheni na mafunzo wa CHADEMA Benson Kigaila na baadhi ya Viongozi wa ngazi ya Mkoa na Wilaya   na Baadhi ya  Wanachama wa Chama hicho.



Akiongea na Wandishi wa Habari Mkoani hapa baada ya kuachiwa kwa Dhamana, Mkurugenzi wa Taifa wa  Operesheni na mafunzo wa CHADEMA Benson Kigaila alisema wao waliwandikia Polisi barua ya kuwataarifu kuwa wana mkutano wa hadhara tarehe 19 mwezi huu kama sheria  ya uchaguzi inavyoelekeza  kuwa utoe taarifa kwa  Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).

Alisema cha kushangaza polisi waliwaletea barua ya kuzuia mkutano wao tarehe hiyo ya Mkutano  majira ya saa 5  na wakati  Jeshi hilo wanajua  wameshaingia gharama za matangazo ya mkutano wao wa hadhara na kukodisha viti pamoja na gari la matangazo .

Kigaila alisema katika barua hiyo ya Polisi ilieleza kuwa sababu za kuuzuia mkutano wa Chadema  ni kuwa Jeshi hilo waligundua kuwa kama mkuutano huo ungefanyika kungekuwa na uvunjifu wa Amani .

Alisema kama Polisi waligundua kuna uvunjifu wa Amani kwa nini Polisi wasilete Askari wengi kulinda Mkutano na matokeo yake walileta gari nne za Jeshi la Polisi kuzuia wanachama wa Chama hicho wasifanye Mkutano si wangetumika kusimamia huo mkutano wakiona kuna jambo linataka kutokea basi wangeuzuia na  kuwahukumu kwa hisia zao

  Akielezea zaidi Kigaila alisema sababu za kukamatwa kwao na Polisi ni  makosa makuu mawili ,moja ni kukiuka Amri halali ya Polisi na lingine ni kutaka kufanya mkutano bila kibali  halali cha Polisi.

Kigaila alisema  chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakiana muda wa kulumbana na Watu wanaotumiwa na vyama vingine kukivuruga chama chao bali wao wanaendel;ea na harakati zao za kutetea maslahi ya Wanyonge .

Mkurungenzi huyo wa CHADEMA alisema wameachiwa kwa Dhamana na hawajui kama Polisi watawafungulia kesi au vipi ila wao kama Chama wanahitaji mkutano wa hadhara kama barua  yao ilivyoomba na hawahitaji kulubana na Jeshi hilo kwani jeshi hilo lipo kwa kuwalinda Watanzania na sio kusababisha vurugu.


mwisho

No comments:

Post a Comment