VIJANA WA KIJIJI CHA NTYUKA KILICHOPO NJE KIDOGO YA MANISPAA YA DODOMA WAKIPELEKA KUUZA KUNI MJINI ILI KUJIPATIA KIPATO. |
Saturday, October 29, 2011
HAYA NI MAISHA YA WATANZANIA
Friday, October 28, 2011
WATEJA MPO WAPI?
Thursday, October 27, 2011
NANI KATI YA HAWA KUIBUKA MLIMBWENDE WA MISS UTALII DOM?
Tuesday, October 25, 2011
UCHOMAJI NYAMA YA KUKU DOM.
Monday, October 24, 2011
Saturday, October 22, 2011
picha tukio la kuvunjwa nyumba njedengwa hapa Dodoma
wakazi wa Njedengwa Manispaa ya Dodoma wakihamisha vyombo vyao baada ya nyumba zao kubomolewa na CDA |
Mabaki ya mabomu yaliyotumiwa na Polisi kuwaondoa wakazi wa Njedengwa Dodoma |
FFU |
Mama ambaye jina lake halikupatina akiwa amezimia baada ya kubomolewa nyumba yake huko Njedengwa Dodoma |
Moja ya majeruhi akisidikizwa na Muuguzi baada ya kujeruhiwa na Polisi katika Zoezi la kuwabomolea Wananchi wa Njedengwa Dodoma |
Polisi akiangalia silaha za asili zilizotumiwa na Wananchi kupambana na waliokuwa wakibomoa makazi yao |
Tinga tinga likibomoa nyumba za Wananchi waliodaiwa kuvamia na kujenga eneo la Mwekezaji Njedengwa Dodoma |
Waandishi wa habari nao walikumbana na mabomu wakati walipokuwa wanatekelza majukumu yao katika tukio la kuvunjiwa nyumba wakazi wa Njedengwa Dodoma,hapa wakinawa uso kupunguza makali ya mabomu |
![]() |
Tingatinga likibomoa moja ya nyumba |
Friday, October 21, 2011
MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA DODOMA
Baadhi ya Waendesha pikipiki wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya kilele cha wiki ya nenda kwa usalama Mkoa wa Dodoma leo katika barabara ya Nyerere |
Blasband ya Jeshi la JKT Makutupora wakiongoza maandamano ya maadhimisho ya kilele cha wiki ya nenda kwa usalama Mkoani hapa leo jioni katika barabara ya Nyerere |
Wanafunzi wa Shule mbalimbali Mkoani hapa wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya kilele cha wiki ya nenda kwa usalama Mkoa wa Dodoma leo |
Thursday, October 20, 2011
VIONGOZI WA CHADEMA WACHIWA NA POLISI DODOMA
PICHA NA IBRAHIM JOSEPH
Tarehe 20/oct/2011
Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 11 waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa wameachiwa kwa Dhamana jana usiku baada ya kuwekewa Dhamana na Wanachama wa Chama hicho .
Viongozi hao walikamatwa jana mchana katika viwanja vya barafu Mkoani hapa na Polisi baada ya kutaka kuanza maandalizi ya mkutano wa hadhara walioumbea kibali tangu tarehe 16 mwezi wa kumi mwaka huu.
Waliokamatwa ni Mkurugenzi wa Taifa wa Operesheni na mafunzo wa CHADEMA Benson Kigaila na baadhi ya Viongozi wa ngazi ya Mkoa na Wilaya na Baadhi ya Wanachama wa Chama hicho.
Akiongea na Wandishi wa Habari Mkoani hapa baada ya kuachiwa kwa Dhamana, Mkurugenzi wa Taifa wa Operesheni na mafunzo wa CHADEMA Benson Kigaila alisema wao waliwandikia Polisi barua ya kuwataarifu kuwa wana mkutano wa hadhara tarehe 19 mwezi huu kama sheria ya uchaguzi inavyoelekeza kuwa utoe taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).
Alisema cha kushangaza polisi waliwaletea barua ya kuzuia mkutano wao tarehe hiyo ya Mkutano majira ya saa 5 na wakati Jeshi hilo wanajua wameshaingia gharama za matangazo ya mkutano wao wa hadhara na kukodisha viti pamoja na gari la matangazo .
Kigaila alisema katika barua hiyo ya Polisi ilieleza kuwa sababu za kuuzuia mkutano wa Chadema ni kuwa Jeshi hilo waligundua kuwa kama mkuutano huo ungefanyika kungekuwa na uvunjifu wa Amani .
Alisema kama Polisi waligundua kuna uvunjifu wa Amani kwa nini Polisi wasilete Askari wengi kulinda Mkutano na matokeo yake walileta gari nne za Jeshi la Polisi kuzuia wanachama wa Chama hicho wasifanye Mkutano si wangetumika kusimamia huo mkutano wakiona kuna jambo linataka kutokea basi wangeuzuia na kuwahukumu kwa hisia zao
Akielezea zaidi Kigaila alisema sababu za kukamatwa kwao na Polisi ni makosa makuu mawili ,moja ni kukiuka Amri halali ya Polisi na lingine ni kutaka kufanya mkutano bila kibali halali cha Polisi.
Kigaila alisema chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakiana muda wa kulumbana na Watu wanaotumiwa na vyama vingine kukivuruga chama chao bali wao wanaendel;ea na harakati zao za kutetea maslahi ya Wanyonge .
Mkurungenzi huyo wa CHADEMA alisema wameachiwa kwa Dhamana na hawajui kama Polisi watawafungulia kesi au vipi ila wao kama Chama wanahitaji mkutano wa hadhara kama barua yao ilivyoomba na hawahitaji kulubana na Jeshi hilo kwani jeshi hilo lipo kwa kuwalinda Watanzania na sio kusababisha vurugu.
mwisho
WANACHAMA WA CHADEMA WAKIANDAMANA
MKUTANO CHADEMA WAKWAMISHWA NA POLISI
Mkurugenzi wa Taifa wa Operesheni wa CHADEMA Benson Kigaila akionyesha barua ya Polisi ambayo waliwapewa kuzuia mkutano wao halali ulikuwa ufanyike juzi jioni |
Tuesday, October 18, 2011
Monday, October 17, 2011
MCHUNGAJI MHANGO ASIMIKWA RASMI KUWA ASKOFU MKUU MSAIDIZI
WAWILI WANAPOAMUA KUACHA UKAPERA!!!
Bw Walter Mnuo na Bi Angela Mndeme wakivishana pete kama ishara ya kufunga pingu za maisha katika kanisa la KKKT -Dodoma Mjini |
Mchungaji Ndosi akimpa mkono wa hongera bwana Harusi Warter Mnuo mara baada ya ibada ya ndoa iliyofungwa mwishoni mwa wiki katika Kanisa la KKKT Dodoma |
Maharusi na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya shughuli hiyo wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa kanisa la KKKT Dodoma |
Sunday, October 16, 2011
ENDELEA KUWA NASI DODOMA LEO
![]() |
Haaaa! agweeeee!!! ushanipiga!!!!!!! ndivyo anavyoonekana huyu mdau katika viwanja vya Nyerere square katika manispaa ya Dodoma |
![]() |
Hii moja ya kona muhimu katika manispaa ya DODOMA |
![]() |
Hapa ndiyo kwa Babu kama wanavyoita vijana wa vyuo vya elimu ya Juu, ambapo utawakuta mishale ya jioni wameanika migongo hapa kupunga upepo huku wengine wakisukumana kwenye ATM upande wa pili!!! |
![]() |
Hapa barabara ya Moja kwa moja kuelekea Bungeni |
![]() |
Hapa ni kiwanja maarufu chaWimp kama hujafika hapa umechelewa, juisi kwa wingi, alamba alamba, hata kushangaa tu inawezekana ama kutega mitego!!!!! |
TEMBELA DUKA LA UREMBO WA MAGARI LA DONS AUTOMOBILE AUTOSPARES AND ACESSORIES BARABARA YA 12
![]() |
Mali mpya kutoka Uingereza, Mashine za kuoshea magari viwanda vidogo na majumbani aina ya Halfords ambazo zinaaminika kuwa na uwezo mkubwa duniani kote!!!!! |
![]() |
Dash board polish inasaidia kutunza sura ya dash board ya gari lako na kukufanya uheshimike mujini!!!! |
DODOMA BENKI ASUBUHI HII HALI IKO HIVI
Subscribe to:
Posts (Atom)